Strawberry jr wa Misri alimpatia mpira Mckinney ambaye alimpasia Farag na kupasiana mpaka kwa Mohamed lakini Farag alipata nafasi ya kupachika pointi tatu na kufunga.
Zikiwa zimesalia dakika 4 kipindi cha kwanza kumalizika, Diogu wa Zamalek alikaribia kikapu na kupachika pointi mbili.
Elsam Mohamed alimpatia mpira Strawberry jr. ambaye alipachika pointi tatu na kusukuma uongozi wa Zalamek hadi pointi tano huku ikiwa imebaki juu kidogo ya dakika moja kumalizia.
Mpira ulichukuliwa na Strawberry jr. alimpatia pasi Diogu ambaye alienda kupachika nyavuni kwa mkono mmoja.
Zikiwa zimesalia dakika 3 kumalizika kwa kota ya tatu, Dieu wa Cobra alikosa kupachika pointi tatu naye Mahmoud wa Zamalek alitokea na kuchukua rebaundi na kumpatia Mboup ambaye aliweka ndani pointi mbili.
Misri ikiwa juu kwa pointi 12 Mckinney alipeleka mpira kwa Farag ambaye alipachika pointi tatu na kuendeleza uongozi wao hadi pointi 15.
Harrington wa Cobra anaweka ndani pointi mbili na kuchezewa vibaya na robo ya tatu inafika mwisho.
Mckinney alimpatia Strawberry jr. ambaye alipita katikati na kufunga huku timu yake ikiongoza kwa tarakimu mbili.
Zikiwa zimesalia juu kidogo ya dakika 5 mchezo kumalizika Sosa wa Zamalek anapachika pointi mbili.
Elsayed akiwa katika mstari wa kurusha mpira wa adhabu alikosa ikiwa imesalia sekunde moja tu, lakini haikubadilisha matokeo huku Zamalek wakiishinda Cobra Sport katika mchezo wa kwanza wa kanda ya Nile kwa jumla ya pointi 80-63.