Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:08

Zaidi ya watu robo milioni wamekufa Corona Marekani, maambukizi yaongezeka zaidi


Idadi ya watu ambao wamekufa nchini Marekani kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona imefikia robo milioni.

Kwa wastani, watu 160,000 wanaambukizwa virusi hivyo kila siku, ikiwa ni ongezeko la asilimia 80 kwa mda wa wiki mbili.

Maambukizi yameongezeka katika majimbo yote 50.

Jumla ya watu 1,155 wanafariki kila siku kutokana na Corona.

Madaktari na wauguzi wanaripotiwa kulemewa na wagonjwa huku makanisa, migahawa, vyumba vya wagonjwa kusubiri huduma ya madaktari na sehemu za kuegesha magari zikigeuzwa na kuwa hospitali ili kuwahudumia wagonjwa.

Wakati huo huo kampuni ya kutengeneza dawa ya Pfizer, imesema kwamba vipimo vya chanjo yake dhidi ya virusi vya Corona vinaonyesha kwamba chanjo hiyo ina ufanisi wa asilimia 95 na pia inawakinga watu wazee dhidi ya kifo kutokana na virusi hivyo.

Kampuni hiyo sasa inatafuta idhini ya kutumia chanjo hiyo kwa matumizi ya dharura wakati maambukizi ya janga la corona yanaendelea kote duniani.

Tangazo la Pfizer na kampuni inayoshirikiana nayo ya BioNTech, limetolewa wiki moja baada ya kutolewa matokeo yanayoonyesha matumaini ya kupatikana chanjo dhidi ya virusi vya Corona.

Kampuni zinazotengeneza chanjo hiyo, zinatarajiwa kuomba ruhusa ya mamlaka ya dawa na tiba nchini Marekani, kuanza kutumia chanjo hizo.

Kampuni ya Pfizer na BioNTech, ilikuwa imesema kwamba chanjo yake ina ufanisi wa asilimia 90.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG