Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 08:09

Zaidi ya watu milioni 1 waambukizwa Corona Afrika kusini


Makaburi katika mji wa Soweto Afrika kusini
Makaburi katika mji wa Soweto Afrika kusini

Haya yanajiri siku chache baada ya maafisa wa afya nchini humo kuripoti kuwepo aina mpya ya virusi vya Corona, vinavyosambaa kwa kasi sana.

Hospitali na vituo vya afya vimeripoti ongezeko kubwa la watu wanaotafuta tiba kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona, huku maafisa wa afya wakiripoti kulemewa na idadi kubwa ya wagonjwa.

Rais Cyril Ramaphosa anatarajiwa kutangaza hatua kali za kuzuia maambukizi zaidi.

Wiki iliyopita, Afrika kusini ilirekodi ongezeko la maambukizi mapya ya virusi vya Corona, kwa wastan, watu 11,700 wakigunduliwa kuambukizwa.

Maambukizi yameongezeka kwa asilimia 39 ikilinganishwa na wiki iliyopita.

Aina mpya ya virusi vya Corona kwa jina 501.V2, inaaminika kuongeza kasi ya maambukizi.

Nchi nyingine za Afrika ambazo zimeathirika sana na maambukizi ya virusi vya Corona ni pamoja na Morocco, Misri, na Tunisia.

XS
SM
MD
LG