Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 00:57

Zaidi ya watu bilioni 1 duniani wana unene wa kupita kiasi-WHO


FILE: Picha hii inaonyesha mtu mwenye unene wa kupita kiasi mjini New York, Mei 8, 2014. Picha ya AP.
FILE: Picha hii inaonyesha mtu mwenye unene wa kupita kiasi mjini New York, Mei 8, 2014. Picha ya AP.

Zaidi ya watu bilioni 1 duniani sasa wanachukuliwa kuwa wanene kupita kiasi, hali inayohusishwa na ongezeko la hatari la matatizo mengi ya kiafya, kulingana na makadirio yaliyosahihishwa na kundi la watafiti wa kimataifa wa shirika la afya duniani (WHO).

Unene uliokithiri umeenea sana na umekuwa jambo la kawaida kuliko kuwa na uzito mdogo katika mataifa mengi, ikiwemo nchi nyingi za kipato cha chini na cha kati ambazo hapo awali zilikuwa zinakabiliwa na utapiamlo.

“Idadi kubwa ya watu wanaishi na unene uliokithiri,” alisema Majid Ezzati, mwandishi mkuu wa makala iliyochapishwa kwenye jarida la The Lancet Alhamisi na muhadhiri kwenye chuo kikuu cha Imperial London.

Matokeo ambayo yanazingatiwa kati ya makadirio ya utafiti huru, yameangazia takwim kutoka kwa zaidi ya watu milioni 220 katika zaidi ya nchi 190.

Forum

XS
SM
MD
LG