Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 19:18

Zaidi ya watu 60 wauawa Mogadishu


Kundi la kigaidi la Al-Shabaab nchini Somalia
Kundi la kigaidi la Al-Shabaab nchini Somalia

Kundi la al-Shabaab lakiri kufanya shambulizi la bomu Mogadishu

Zaidi ya watu 60 wameuawa Jumanne katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, na wengine zaidi ya 15O kujeruhiwa baada ya gari lililotegwa bomu kulipuliwa kwenye uwanja wa wizara ya elimu. Kundi la wanamgambo la al-Shabab limekiri kuhusika na shambulio hilo likisema lililenga serikali ya mpito ya Somalia na walinda amani wa Umoja wa Afrika wanaoisaidia serikali hiyo. Walioshuhudia waliiambia idhaa ya Kisomali ya Sauti ya Amerika kuwa watu wawili waliojitoa mhanga waliendesha gari hilo hadi kwenye mlango wa uwanja huo na kulipua bomu hilo saa tano asubuhi saa za Somalia. Taarifa ya serikali ilisema waliouawa ni 15 lakini waandishi habari waliokuwepo katika eneo la shambulizi hilo walisema maafisa wa polisi na wafanyikazi wa afya walihesabu zaidi ya maiti 60. Maafisa katika hospitali za Medina na Bandir waliiambia Sauti ya Amerika kuwa wamepokea zaidi ya watu 147 waliojeruhiwa katika shambulizi hilo.

XS
SM
MD
LG