Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 10:27

Zaidi ya watu 5,700 wamefariki kutokana na Ebola Afrika Magharibi


Timu ya wafanyakazi wa afya kutoka Cuba ikiwa Freetown, Sierra Leone Nov.17,2014

Takwimu mpya zilizotolewa Jumatano na shirika la afya duniani (WHO) zinaonyesha kwamba idadi ya waliofariki iliongezeka kwa 230 tangu ripoti ya shirika hilo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Takriban 5,700 wamefariki dunia mpaka sasa kutokana na ugonjwa wa Ebola huko Afrika magharibi, huku kukiwa na ishara kwamba kusambaa kwa ugonjwa kunapungua lakini hakujaisha.

Takwimu mpya zilizotolewa Jumatano na shirika la afya duniani (WHO) zinaonyesha kwamba idadi ya waliofariki iliongezeka kwa 230 na kufikia 5,689 tangu ripoti ya shirika hilo mwishoni mwa wiki iliyopita. Idadi hiyo iliongezeka kutokana na kesi 15,935 za maambukizo ya Ebola, ongezeko la kiasi cha 600.

Shirika hilo la Umoja wa mataifa linasema idadi ya kesi mpya zilizoripotiwa ni thabiti huko Guinea na zimepungua huko Liberia lakini inaweza kuongezeka huko Sierra Leone, ambako kumeripotiwa kesi mpya theluthi mbili.

WHO inaripoti kesi 8 za Ebola nchini Mali ambapo watu sita wameshafariki.

XS
SM
MD
LG