Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 23:12

Zaidi ya watu 50 wauwawa Nigeria


Magari yaliochomwa kwenye shambulizi la awali Nigeria. Picha ya maktaba
Magari yaliochomwa kwenye shambulizi la awali Nigeria. Picha ya maktaba

Dazeni ya watu waliokuwa kwenye pikipiki wameshambulia kijiji na kuua zaidi ya watu 50 katika tukio la karibuni kabisa kaskazini mwa Nigeria wakazi wamesema Jumapili.

Kundi hilo limekuwa likisumbua maeneo ya kaskazini magharibi katika miaka hivi karibuni, na kusababisha maelfu ya watu kukimbia na kupata umaarufu wa kidunia kutokana na kuteka watu katika shule na kutaka fedha ili kuachilia mateka.

Mzee mmoja wa eneo hilo Abdullahi Karman Unashi ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba watu hao waliingia katika kijiji cha Dankade katika jimbo la Kebbi siku ya Ijumaa usiku na kufyatuliana risasi na wanajeshi pamoja na polisi.

Vikosi vya usalama vililazimishwa kujipanga na kuacha kundi hilo likichoma maduka na mashamba ya nafaka pamoja na mifugo katika saa za awali za Jumamosi alieleza mkazi huyo.

XS
SM
MD
LG