Polisi wa eneo hilo walisema Ijumaa jioni kwamba watu 48 walikufa katika msongamano wa magari ya kawaida, mabasi madogo, pikipiki na malori katika eneo la Londiani.
“Moyo wangu umepata msikitiko makubwa,” Gavana wa Kaunti ya Kericho, Erick Mutai, aliandika katika ukurasa wa mtandao wa Facebook.
Shirika la msalaba mwekundu la Kenya imeliambia shirika la habari la AFP kuwa mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha ilizuia shughuli ya uokoaji.
Rais wa Kenya William Ruto aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter, “Nchi inaomboleza pamoja na familia ambazo zimepoteza wapendwa wao katika ajali mbaya ya barabarani Londiani.”
Forum