Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 20:34

Zaidi ya watu 5,500 bado hawajulikani waliko katika eneo lililokumbwa na mafuriko mashariki ya Congo


Uharibifu uliosababishwa na mafuriko mjini Goma, DRC.
Uharibifu uliosababishwa na mafuriko mjini Goma, DRC.

Zaidi ya watu 5,500 bado hawajulikani waliko katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya  Kidemokrasia ya Kongo, ambako mafuriko yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 400, afisa mmoja wa serikali katika eneo hilo alisema Jumanne, wakati manusura wakisubiri msaada wa chakula.

Miili ya watu wengi imepatikana kutoka katika vijiji vya Bushushu na Nyamukubi katika jimbo la Kivu Kusini, eneo la Kalehe, tangu mvua kubwa iliyonyesha kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi siku ya Alhamisi, na kuharibu majengo na kuosha mazao.

Makaburi yaliyozikwa watu wengi yalichimbwa mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuwazika waliofariki, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto, jambo lililozua malalamiko kutoka kwa baadhi ya asasi za kiraia wakisema maziko hayo hayakuwa na heshima.

Wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu wametoa tahadhari kuhusu ukosefu wa vifaa vya kuwasaidia zaidi ya wakazi 8,800 walioathirika, wengi wao wakiwa wameachwa bila makazi huku wakiwa na kiwewe baada ya mojawapo ya maafa mabaya zaidi ya kiasili katika historia ya hivi karibuni ya Kongo.

Afisa mmoja wa serikali alisema Jumanne kuwa maiti 411 zimepatikana hadi sasa na kwamba takriban watu 5,525 bado hawajapatikana.

XS
SM
MD
LG