Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 23:18

Zaidi ya watu 400 wameuawa kati ya Januari na Machi nchini Sudan Kusini-UN


Mkuu wa tume ya Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini, Nicholas Hayson, akizungumza na waandishi wa habari mjini Juba, Mei 24, 2023.

Zaidi ya watu 400 waliuawa nchini Sudan Kusini kati ya mwezi Januari na Machi mwaka huu, huku mapigano kati ya makabila yakichangia zaidi kwa ghasia hizo zinazolikumba taifa hilo, ripoti ya Umoja wa mataifa imesema Ijumaa.

Mapigano yalizuka mkesha wa Krismasi mwaka jana wakati watu wenye silaha kutoka jimbo la Jonglei waliposhambulia jamii katika eneo jirani la Greater Pibor, huku ghasia zikienea baadaye katika maeneo mengine ya nchi.

“Ghasia zinazosababishwa na wanamgambo wa kijamii na makundi ya kulinda raia zimekuwa chanzo kikuu cha ghasia zinazoathiri raia”, ofisi ya Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) ilisema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Ofisi hiyo imesema “ Kuanzia Januari hadi Machi 2023, ilichunguza matukio 920 ya ghasia dhidi ya raia wakiwemo watoto 243, ambapo raia 405 waliuawa, 235 walijeruhiwa, 266 walitekwa nyara, na 14 ambao walitendewa ukatili wa kingono unaohusiana na mzozo.”

Wachunguzi waliorodhesha pia mauaji 22 ya kiholela kati ya Januari na Mei mwaka huu,” yanayodaiwa kufanywa na maafisa wa usalama wa Sudan Kusini,” taarifa yao imesema.

Forum

XS
SM
MD
LG