Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 09:14

Zaidi ya watu 40 wamefariki dunia  kutokana na maandamano Peru


Waandamanaji wanaopinga serikali waliposhiriki katika msafara wa pikipiki huko Juliaca, Peru, Jumatatu, Januari 30, 2023.
Waandamanaji wanaopinga serikali waliposhiriki katika msafara wa pikipiki huko Juliaca, Peru, Jumatatu, Januari 30, 2023.

Wabunge nchini Peru wameahirisha mjadala kuhusu pendekezo la Rais aliye matatani Dina Boularte la kupanga uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu.

Bunge lilipanga kujadili pendekezo hilo siku ya Jumatatu, lakini bunge hilo lilitoa taarifa kwamba mjadala umesogezwa hadi Jumanne.

Pendekezo la kusogeza uchaguzi uliopangwa kufanyika mwaka wa 2026 hadi Aprili 2024 limevutia uungwaji mkono unaoongezeka katika Bunge lakini Rais Boularte anawashinikiza wabunge kuidhinisha pendekezo lake ili kuzima machafuko makubwa yaliyosababishwa kuondolewa madarakani kwa mtangulizi wake, Pedro Castillo Desemba mwaka jana baada ya kujaribu kuvunja bunge.

Boularte alisema Jumapili ikiwa pendekezo lake litakataliwa atapendekeza marekebisho ya katiba ya Peru ili uchaguzi ufanyike mwezi Oktoba.

Maandamano hayo yamesababisha vizuizi mitaani ambavyo vimesababisha uhaba wa chakula, mafuta na vifaa vingine vya msingi kote Peru.

Zaidi ya watu 40 wamefariki dunia kutokana na maandamano hayo, akiwemo muandamanaji mmoja aliyefariki katika mji mkuu wa Lima siku ya Jumamosi baada ya kupokea kile ambacho maafisa wanasema ni pigo kichwani.

XS
SM
MD
LG