Vikosi vya usalama vilifyatua gesi ya kutoa machozi wakati waandamanaji wa Sudan wakiandamana katika mji mkuu Khartoum siku ya Jumapili dhidi ya uongozi wa jeshi la nchi hiyo, ukiushikilia kuhusika na kuzuka kwa ghasia katika Jimbo la Blue Nile.
Zaidi ya watu 30 waliuawa na 100 kujeruhiwa katika mapigano ya kikabila yaliyoanza wiki iliyopita kati ya makabila ya Hausa na Fung katika jimbo la kusini mashariki, karibu na mpaka na Ethiopia, kulingana na maafisa wa Sudan na Umoja wa Mataifa.
Mamlaka ilisema Jumapili itaimarisha usalama katika jimbo hilo na kuchunguza mapigano hayo. Amri ya kutotoka nje imetangazwa katika miji miwili.