Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 20:37

Zaidi ya watu 10 wauawa mashariki mwa DRC


Ramani ya DRC, jimbo la Ituri
Ramani ya DRC, jimbo la Ituri

Machafuko mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu kumi katika siku tatu, vyanzo vya kijeshi na vya eneo hilo vimesema Jumapili.

Zaidi ya makundi ya wanamgambo 120 yamesambaa mashariki mwa DRC, na kuna mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya raia.

Wanajeshi 2 ni miongoni mwa waliouawa tangu Ijumaa.

Kiongozi wa kijeshi katika jimbo la Kivu Kaskazini amesema Jumapili “Tumempoteza mwanajeshi shujaa katika shambulio dhidi ya ngome yetu katika kitongoji cha kaskazini mwa mji wa Butembo lililofanywa na wanamgambo wa Mai-Mai”.

Kiongozi huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema wanamgambo wawili wa kundi hilo waliuawa.

Katika jimbo la kaskazini mashariki la Ituri, wachimba dhahabu 6 wameuawa Jumapili na kukatwa vichwa na waasi wa kundi la CODECO, Prince Kaleta, ambaye ni kiongozi wa shirika la kiraia huko Lodjo, Ituri ameliambia shirika la Habari la AFP.

CODECO ni kundi la kisiasa na kidini ambalo linadai kuwakilisha maslahi ya watu kutoka kabila la Lendu.

Linachukuliwa kama moja ya makundi ya wanamgambo yanayofanya ukatili, na linashtumiwa kwa mauaji ya kikabila huko Ituri.

Raia watatu waliuawa Jumamosi usiku katika shambulio lilofanywa na waasi wa kundi la ADF huko Kivu Kaskazini, amesema Flavien Kakule, mkuu wa mtaa katika eneo la utawala wa Bashi, wilaya ya Beni.

XS
SM
MD
LG