Kumekuwepo na mashambulio 617 ya halaiki nchini Marekani kuanzia Januari mwaka 2022 hadi mwisho wa Novemba ikiwa ni ongezeko la karibu asili mia 50 kulingana na mwaka 2014, kufuatana na takwimu za taasisis ya Gun Violence Archive GVA.
Idadi ya mauwaji hayo ya halaiki ambayo na zaidi ya watu wane kwa mara moja imeongezeka sana na hata kua kama jambo la kawida kulingana na GVA
Takwimu hizo zinaonesha zaidi ya watu elfu 3 waliuliwa katika mauwaji ya halaiki pekee yake na kwa jumla mwakla huu kuna watu elfu 40 498 walouliwa kutokana na bunduki Marekani
Takwimu hizi zinatia wasi wasi wamarekani wengi na hasa wanafunzi wanaharakati wazazi na baadhi ya wanasiasa wanataka hatua kali zichukuliwe kudhibiti bunduki kubwa za mashambulizi.
Facebook Forum