“Wengi wana njaa, wamechoka na wanahitaji msaada wa haraka,” alisema Filippo Grandi kwenye mtandao wa kijamii.
Grandi aliongeza kuwa “ UNHCR na washirika wengine wa kutoa misaada ya kibinadamu wameongeza msaada wao kwa mamlaka za Armenia, lakini msaada wa kimataifa unahitajika kwa haraka.”
Jeshi la Azerbaijan wiki iliyopita lilivamia na kuchukua udhibiti wa eneo linalokaliwa na watu wa kabila la Armenia na kusababisha wimbi la ghafla la wakimbizi.
Armenia Jumamosi imesema zaidi ya watu 100,000 kati ya idadi ya watu wanaokadiriwa kuwa sawa na 120,000 walikimbia tangu eneo hilo lililojitenga kushuhudia mapigano dhidi ya utawala wa Azerbaijan kwa miongo kadhaa, na mapigano hayo kumalizika ghafla kwa kushindwa.
Forum