Zaidi ya wafanyakazi wa zima moto 600, ikiwa ni pamoja na misaada kutoka nchi kadhaa za Ulaya wakisaidiwa na ndege kadhaa zinazomwaga maji na helikopta wanapambana na mioto mikubwa mitatu ya msituni inayoendelea Ugiriki, miwili kati yao ikiendelea kwa siku kadhaa.
Moto mkubwa katika mikoa ya kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo ya Evros na Alexandroupolis, unaaminika kusababisha vifo vya watu 20, unawaka kwa siku ya tisa.
Moto mwingine mkubwa ulikuwa ukiwaka kwa siku kadhaa kwenye miteremko ya Mlima Parnitha, kwenye ukingo wa kaskazini-magharibi mwa mji mkuu wa Ugiriki, wakati moto wa tatu ulianza Jumamosi kwenye kisiwa cha Cycladic cha Andros na bado ulikuwa ukiwaka bila udhibiti siku ya leo Jumapili.
Forum