Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 08, 2025 Local time: 10:16

Zaidi ya robo ya raia wa Syria wanaishi katika umasikini uliokithiri


Zaidi ya robo ya Wasyria wanaishi katika umaskini uliokithiri, Benki ya Dunia imesema Jumamosi, ikiwa ni miaka 13 katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoharibu uchumi na kufanya mamilioni ya watu kuwa maskini.

Benki ya Dunia ilichapisha ripoti mbili mpya kuhusu Syria, ambayo iligundua kuwa asilimia 27 ya Wasyria, takriban milioni 5.7 wanaishi katika umaskini uliokithiri, ambao haukuwepo kabla ya mzozo, uliathiri zaidi ya Msyria mmoja kati ya wanne mwaka 2022 na huenda ukazidi baada ya tetemeko kubwa la ardhi mwaka jana moja ya ripoti imesema.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, karibu asilimia 90 ya Wasyria wanaishi katika umaskini, wakati hapo awali ilikadiria kuwa karibu milioni mbili waliishi katika umaskini uliokithiri baada ya zaidi ya muongo mmoja wa vita.

Forum

XS
SM
MD
LG