Jean Pierre Bikilisende, afisa kwenye eneo la vijijini la Mungwalu wilayani Djugu, katika mkoa wa Ituri, amesema wanamgambo wa kundi la CODECO walifanya shambulio hilo kwenye mgodi huo.
Bikilisende amesema wanamgambo hao waliushambulia mgodi wa dhahabu wa Camp Blanquette na kwamba maiti 29 ziliondolewa huko, huku maiti nyingine sita zilizochomwa moto zimekutwa zimezikwa kwenye eneo hilo.
Miongoni mwa waliouawa kuna mtoto mwenye umri wa miezi minne, ameongeza.
Cherubin Kukundila, kiongozi wa kiraia huko Mungwalu, amesema takriban watu 50 waliuawa katika shambulio hilo.