Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 13:27

Raia waendelea kuteseka kutokana na mzozo nchini Yemen


Watoto nchini Yemen wakielekea kutafuta maji
Watoto nchini Yemen wakielekea kutafuta maji

Kwa mujibu wa kundi la madkatari wasio na mpaka MSF raia wanaendelea kuathirika na ghasia katika mji wa Taiz nchini Yemen, licha ya sitisho la mapigano ambalo lilifikiwa miezi miwili iliyopita baina ya pande zinazozozana.

Baadhi ya mapigano makali na upigaji makombora umefanyika katika maeneo yenye wakazi wengi ya Taiz, huku makombora ya kila siku, mashambulizi ya anga, milipuko ya mabomu, milipuko ya mabomu ya kutegwa ardhini na mashambulizi ya walenga shabaha, kundi hilo la misaada ya kiafya limesema jana na kuongezea kuwa mapigano na upigaji makombora unafanyika katika maeneo yenye raia wengi mjini humo.

Hakuna upande unaozozana unaonekana kufanya juhudi za kujuia majeruhi miongoni mwa raia, taarifa hiyo ilisema.

MSF imezitaka pande zote katika mzozo wayemen huo kuchukuwa hatua kubwa kuwalinda raia, kupunguza kiwango cha mzozo na kufungua njia ya kufanikisha upelekaji misaada ya kibinadam huko Taiz.

Mjumbe maalum wa umoja mataifa kwa yemen, Ismail Ould Cheik Ahmad alikutana katika muundo wa mashauriano ya amani na wapatanishi waandamizi wa yemen wanaoshiriki katika mazungumzo ya amani ya Yemen nchini Kuwait.

XS
SM
MD
LG