Kiongozi wa kundi lenye sera kali Anwar al-Awlaki aliyeuwawa na shambulizi la Marekani nchini Yemen Ijumaa alikuwa maarufu ndani ya al-Qaida na ni kiongozi wa mtandao wa ugaidi nchini Yemen.
Utawala wa Obama ulimlenga Awlaki, raia wa Marekani, kwa kazi zake zilizolenga kuongoza ugaidi dhidi ya Marekani. Alikuwa maarufu zaidi tangu kutokea kifo cha mkuu wa al-Qaida, Osama bin Laden mwezi Mei.
Awlaki ambaye kundi lake nchini Yemen linajulikana kama al-Qaida katika peninsula ya kiarabu, inaaminika alilengwa katika shambulizi la ndege moja ya Marekani isiyokuwa na rubani mwezi Mei ambapo iliwauwa washukiwa wanamgambo wawili nchini Yemen. Pia aliepuka shambulizi moja la anga ambalo liliwauwa watu 30 mwaka jana.
Awlaki alizaliwa katika jimbo la New Mexico nchini Marekani mwaka 1971 ambapo wazazi wake walikuwa wahamiaji kutoka Yemen na alikuwa akizungumza kwa ufasaha lugha ya kiarabu na kiingereza.
Alikuwa Imam katika misikiti kadhaa ya Marekani ukiwemo mmoja huko magharibi ya mji wa San Diego ambao uliongozwa na watu wawili ambao baadae walihusika katika mashambulizi ya ugaidi ya Septemba 11, 2001 dhidi ya Marekani.
Baada ya Awlaki kusafiri kuelekea Yemen alikuwa mhubiri kwa njia ya mtandao na akiwa na wafuasi wakiwemo viongozi wengi wa waasi duniani kote ambao walisikiliza hotuba zake zilizorekodiwa.
Licha ya kuwa m-Marekani, Awlaki alikuwa mkosoaji wa Marekani na alishukiwa kuwashawishi watu wengine kuhusika na ghasia dhidi ya maslahi ya Marekani. Katika hotuba yake ya Novemba mwaka 2010, aliwaambia wafuasi wake wanatakiwa wajihisi huru kuwauwa wamarekani mahala popote, wakati wowote, bila ya kuhitaji ushauri wa mtu yeyote. Awlaki alisema waislam wanazungumza na uso wa wa-Marekani katika hali ya sisi au wao.
Awlaki alikuwa akitafutwa na Marekani na Yemen kwa kuhusika kwake katika mashambulizi kadhaa ya ugaidi.
Kiongozi wa kundi lenye sera kali Anwal al-Awlaki aliuwawa Ijumaa katika shambulizimoja la Marekani nchini Yemen