Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 04:03

Maandamano zaidi yafanyika Yemen


Maandamano dhidi ya utawala wa miaka 32 wa Rais Ali Abdullah Saleh wa Yemen.
Maandamano dhidi ya utawala wa miaka 32 wa Rais Ali Abdullah Saleh wa Yemen.

Wanaharakati wa upinzani huko Yemen wanaendelea na maandamano yao dhidi ya Rais Ali Abdullah Saleh, siku moja baada ya majeshi ya usalama yalipovamia eneo la chuo kikuu cha sana’a, na kumuuwa mtu mmoja na kujeruhi wengine kadhaa.

Wakiwa wamekasirishwa na uvamizi wa serikali, ambao ulitumia silaha za moto na gesi ya kutoa machozi, waandamanaji zaidi walijitokeza hapo Jumatano kuzunguka chuo kikuu. Waandamanaji waliahidi kuendelea na hatua yao hadi wanauondoa madarakani utawala wa Rais uliodumu kwa miaka 32.

Mjini Washington, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Mark Toner, Jumatano aliisihi serikali ya Yemen kufanya uchunguzi na kumuwajibisha yeyote ambaye huenda alitumia nguvu kupita kiasi. Kundi la haki za binadamu la Amnesty International, pia lililaani shambulizi hilo ambalo liliwajeruhi watu 80.


XS
SM
MD
LG