Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 08:42

Saudia Arabia yasitisha mashambulizi ya anga Yemen


The waning moon sets behind leafless sumac trees on a crisp, clear morning in Portland, Maine.
The waning moon sets behind leafless sumac trees on a crisp, clear morning in Portland, Maine.

Saudi Arabia imesema inasitisha mashambulizi ya anga ya muungano wa kiarabu dhidi ya wa Houthi nchini Yemen lakini haitapunguza shinikizo kwa waasi.

Maafisa kutoka Saudi Arabia wamesema Jumanne kwamba baada ya wiki nne za mashambulizi ya mabomu, wa Houthi siyo tishio tena kwa raia wa Yemen au hata mataifa mengine ikiwemo Saudi Arabia. Wamesema kwamba juhudi za ushirika kuwazuia waasi kusonga mbele na kuirejesha serikali ya Yemen inayotambuliwa kimataifa zinaingia awamu mpya, wakilenga kwenye utaratibu wa kisiasa na kuwasaidia raia.

Wakati huohuo,Saudi Arabia imesema muungano utaendelea kuwazuia wanamgambo wa kihouthi kuzunguka kote nchini na kwamba mashambulizi ya anga yanaweza kurejelewa wakati wowote. Iran inayoshukiwa kuwapa waasi wa ki Houthi silaha wameliita tangazo hilo la Saudi Arabia kuwa ni hatua inayofaa kuelekea suluhisho la kisiasa.

XS
SM
MD
LG