Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 22:13

WHO kuanza kampeni dhidi ya homa ya manjano mwezi huu


Mbu aina ya Aedes aegypti anaesambaza virusi vya homa ya manjano na zika, katika maabara ya taasisi ya sayansi hukoInstitute at Sao Paulo Brazil.
Mbu aina ya Aedes aegypti anaesambaza virusi vya homa ya manjano na zika, katika maabara ya taasisi ya sayansi hukoInstitute at Sao Paulo Brazil.

Idara ya afya duniani WHO, inaongoza kampeni kubwa ya chanjo ya homa ya manjano huko Afrika ya kati ili kuzuia kuenea kitaifa na kimataifa kwa ugonjwa huo mbaya. Kampeni hiyo inayoanza mwezi huu, inalenga kutowa chanjo kwa watu takriban millioni 15.5 huko Angola na Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Homa ya manjano iliibuka mwishoni mwa mwaka jana katika mji mkuu wa Angola, Luanda, na haraka kuenea katika nchi jirani ya jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Kampeni hiyo ya miezi 2 inafanywa kabla ya kuanza kwa msimu wa mvua ujao hapo September, pale mbu wanapozidi na maambukizo kuzidi kuenea.

Bruce Aylward, mkurugenzi mtendaji katika idara ya maambukizo na dharura za kiafya kwenye shirika la WHO, anasema kuibuka kwa ugonjwa huu ni hatari kwa sababu inatokea katika miji mikubwa.

Anasema kuzuka kwa kesi nyingi za homa ya manjano katika maeneo ya mijini inatokea kwa sababu mbu wanaweza kuambukiza maelfu ya watu kwa haraka zaidi.

Alywald anasema, kusambaa ugonjwa huo na kuongeza kesi zilizopo, utaona kiwango kikubwa cha vifo. Hii inaweza kuwa hatari sana na kuharibu shughuli. Lakini tatizo jengine linalotia wasiwasi ni pale maambkizo yakitokea katika miji mikubwa, kunaleta hatari ya kuenea virusi hivyo kwa nchi za kimataifa.

Alywald anasema kesi mbili ziloripotiwa huko Kenya na kesi nyengine 11 huko China, zilitokana na wanaume wa kichina ambao walikuwa wakifanya kazi huko Angola. Homa ya manjano ni sugu katika nchi 47, ambzo 33 miongoni mwa hizo , ziko barani Afrika. Nyengine ziko Amerika ya kusini.

Homa ya manjano ni viusi ambavyo katika kesi mbaya, inaweza kuathiri ini la binadam , kusababisha ngozi kuwa na rangi ya manjano. Mbu anaeenza virusi hivyo ni Aedes Aegypti, mbu yuleyule anae eneza virusi vya Zika. Kwa vile mbu anapatikana pia huko Asia, Bw. Alywald anaonya uwezekano wa kuibuka kwa mzozo wa kimataifa upo.

Hata hivyo Alywald aliiambia VOA kuwa ubashiri wa kudhibiti kuenea kwa Homa ya manjano ni mzuri.

Alywald anasema, hii si kama Ebola au Zika, magonjwa mabyao hatuna chanjo ya kudhibiti. Huu ni ugonjwa ambao tuna chanjo yake na kuna sheria chini ya kanuni za kiafya za kimatiafa kuwa na chanjo ya homa ya manjano. Kwa hiyo baadhi ya shughuli zetu nan chi ziloathirika na ugonjwa huo ni kuhakikisha kuwa wana sera za chanjo kwa wasafiri.

Takwimu za hivi karibuni za WHO zinaonyesha kuwa kuna takriban zaidi ya elfu 3 mia 5 na zaidi ya kesi 860 zimethibitishwa za homa ya manjano huko Angola, na kadhalika vifo takriban mia 355. Nchini DRC kumekuwa na kesi zinazotuhumiwa elfu 1 mia 3, kesi 68 zilothibitishwa ba vifo 75.

Gharama za kampeni kubwa ya homa ya manjano inatarajiwa kufika dola millioni 34. Alywald anasema WHO itatowa wito wa dola millioni 20 katika siku zijazo, huku Angola na DRC zikijazia.

XS
SM
MD
LG