Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 13, 2025 Local time: 12:41

Rais wa Namibia asema Ya Toivo atazikwa kitaifa


Rais Hage Geingob
Rais Hage Geingob

Shujaa na mpigania uhuru, Herman Andimba Toivo ya Toivo atazikwa kwa heshima zote za kitaifa huko Namibia, Rais Hage Geingob ametangaza wiki hii.

Akizungumza na waombolezaji katika makazi ya Ya Toivo huko Windhoek, Rais amesema habari zaidi za mipango ya mazishi yake zitatolewa baada ya kushauriana na familia ya marehemu. Ya Toivo aliaga dunia siku ya Ijumaa, akiwa na miaka 92..

Alikuwa mwanaharakati mwenye kupinga ubaguzi wa rangi, mwanasiasa na mfungwa wa kisiasa aliyekuwa mstari wa mbele wakati wa harakati za ukombozi kabla ya uhuru wan nchi hiyo.

Ya Toivo ni moja wa waasisi wa chama cha kupigania uhuru cha Swapo (South West African People’s Organisation) katika miaka ya 60 na chama kilikongwe kilichokuwa kinajulikana kama Ovamboland People’s Organisation (OPO) mwaka 1959.

Founding President Sam Nujoma, Former President Hifikepunye Pohamba and his wife Muasisi Rais Sam Nujoma, Rais mstaafu Hifikepunye Pohamba na mkewe Penehupifo Pohamba, Waziri Mkuu Saara Kugongelwa-Amadhila na mama wa taifa Monica Geingos walikuwa kati ya waombolezaji waliohudhuria maombi maalum nyumbani kwake Ya Toivo. Ya Toivo ameacha mke, Vicky, na watoto mapacha.

XS
SM
MD
LG