Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 22:47

Xi Jinping azuru Hong Kong kwa maadhimisho ya miaka 25


Rais wa China Xi Jinping awasili Hong Kong kwa maadhimisho ya 20 tangu kutoka mikononi mwa Uingereza
Rais wa China Xi Jinping awasili Hong Kong kwa maadhimisho ya 20 tangu kutoka mikononi mwa Uingereza

Rais wa China Xi Jinping Alhamsi amewasili Hong Kong kabla ya maadhimisho ya miaka 25 tangu mji huo ulipochukuliwa na taifa lake kutoka Uingereza.

Xi amewasili mjini humo kwa treni ya mwendo kasi, ikiwa ni safari yake ya kwanza nje ya China bara tangu kuzuka kwa janga la corona. Wakati akiandamana na mke wake Peng Liyuan pamoja na waziri wa mambo ya kigeni Wang Yi, Xi Jinping amelakiwa na watoto wa shule waliokuwa wakipeperusha vibendera pamoja na mashada ya maua, huku kukiwa na wacheza dansi maalum pamoja na vyombo vya habari vilivyo alikwa.

Ziara hiyo iliwekwa siri kwa muda wakati hali ya usalama ikiimarishwa mjini humo. Baadhi ya viongozi wa serikali ya wamezuiliwa kuhudhuria sherehe hizo za Ijumaa kwa kigezo cha kuzuia maambukizi ya corona, huku baadhi ya wanahabari wakizuiliwa kuhudhuria maadhimisho hayo, yatakayoonyesha udhibiti wa chama tawala cha kikomunisti cha China kwenye mji huo.

XS
SM
MD
LG