Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 03:37

Timu 3 za Afrika katika Kombe la Dunia 2010


Mashabiki wa Nigeria wakiandamana kupitia mtaa wa Hillsborough Johannesburg kabla ya timu yao kushuka kwa mchuano wa kwanza.
Mashabiki wa Nigeria wakiandamana kupitia mtaa wa Hillsborough Johannesburg kabla ya timu yao kushuka kwa mchuano wa kwanza.


ALGERIA

Algeria ipo kwenye kundi la C pamoja na Marekani, Uingereza na Slovania. Imemaliza miaka 24 tangu ishiriki kwa mara ya mwisho katika fainali za kombe la dunia tangu Mexico mwaka 1986. Algeria ilianza kupotea katika ramani ya soka na kuanza kidogo kujenga upya timu yao na hatimaye kurejea katika kiwango cha juu.
Wachezaji wa sasa wa timu hiyo wanajiona wana ari kubwa kuliko awali na wanaamini kuwa wanaweza kutoa upinzani mkali nchini Afrika Kusini.

Walivyofuzu.
Algeria walifanikiwa kufuzu baada ya kucheza mara mbili dhidi ya Misri na hatimaye ikafanikiwa katika mchezo wa marudiano ambao ulichezwa katika uwanja wa Khartoum baada ya kufungana kwa kila kitu katika mechi za awali lakini Algeria wakafuzu baada ya kuifunga Misri bao moja kwa bila novemba 18 mwaka jana.
Algeria ilifuzu na kuziacha Zambia na Rwanda zikiwa pointi kumi na moja nyumas yake.

Wachezaji nyota.
Mfungaji wa bao lililowapeleka Afrika Kusini Antar Yahia ni mmoja wa mihimili muhimu wa timu hiyo katika safu ya ulinzi akishirikiana na Madjid Bougherra, Nadir Belhadj na mlinda mlango Lounes Gaouaoui, licha ya kwamba msaidizi wake Fawzi Chaouchi anafanya vyema hivi sasa na huenda akarejea langoni.
Nahodha Yazid Mansouri ambaye anacheza sehemu yab kiungo ni nmchezaji hatari akiwalisha mipira washambuliaji Karim Ziani na Mourad Meghni ambao wanaweza kuleta madhara wakati wote. Mwisho ni mshambuliaji Karim Matmour.
Kocha: Rabah Saadane raia wa Algeria ambaye ni kocha pekee mwafrika.

Rekodi:
Wamewahi kutwaa ubingwa wa kombe la mataifa ya Afrika mara moja - mwaka 1990.

NIGERIA

Nigeria ipo kwenye kundi B pamoja na Argentina,Ugiriki na Jamhuri ya Korea, matumaini ya timu hii yalikuwa madogo katika sku za nyuma kuhusu nafasi ya Nigeria katika fainali hizi za Afrika Kusini lakini katika siku za karibuni hali imebadilika na timu hii inaoenekana inaweza kumaliza mashindano haya miongoni mwa timu nne bora. Licha ya kwamba katika mashindano yaliyopita ya kombe la dunia kumbukumbu zinaonyesha kuwa Nigeria imewahi kuambulia pointi moja tuu katika michezo mitano ya fainali za kombe la dunia iliyowahi kucheza na pia katika fainali zilizopita nchini Ujerumani mwaka 2006 haikupata nafasi lakini timu hilo maarufu barani afrika linatarajiwa kutoa ushindani mkubwa katika fainali hizo na kuwa kivutio kikubwa.

Hali hii inachagizwa na fainali za mwaka 1994 nchini Mrekani ambapo Nigeria ilianza kwa kishindoi baada ya kuifunga Bulgaria 3-0 katika mechi ya awali lakini baadae ikafungwa mabao 2-1 na Italy katika raundi ya pili. Lakini Nigeria ya wakati huo ilikuwa na nyota kama Sunday Oliseh, Victor Ikpeba, Jay-Jay Okocha na Finidi George ambao walikuwa maarufu na kweli walionyessha dhahiri kutetea taifa na bara la Afrika. Lakini pia hata kipigo walichokitoa kwa Spain cha mabao 3- 2 mwaka 1998 na Bulgaria 1-0 yalitoa nafasi kwa Nigeria kuonekana kama taifa linalotisha katika soka duniani.

Walivyofuzu:
Nigeria walifuzu licha ya kuanza vibaya kwa kutoka sare na Msumbiji na wakawa na kazi ya kufukuzana na Tunisia hadi siku ya mwisho ya michezo ya kufuzu ambapo Tunisia walifungwa bao moja kwa bila na Msumbiji na Nigeria wakaifunga Kenya mabao 3-2 na hivyo kufuzu baada ya Obafemi Martin alikuwa shujaa ambapo aliingia kipindi cha pili na kusawazisha bao na baadae kufgunga bao la ushindi na kufunga bao la ushindi na kuipatia nchi yake tikiti ya kufuzu.

Wachezaji nyota.
Nigeria ama The Super Eagles kama wanavyofahamika wana uwezo wa kufunga magoli mengi katika fainali hizi za Afrika Kusini. Washambuliaji kama Obafemi Martins, Yakubu Aiyegbeni, Peter Odemwingie na wachezaji chipukizi Victor Obinna na Ikechukwu Uche na hata mkongwe Nwankwo Kanu ambaye anaonekana fainali hizi zitakuwa ndio za mwisho kwake, wanaweza kuipatia ushindi timu yao wakati wowote bila kujali wanacheza na nani. Sehemu ya kiungo ya Nigeria inaundwa na Jon Obi Mikel wakati ulinzi wapo Joseph Yobo na Tye Taiwo .
Kocha: Lars Lagerback raia wa Sweden.

Rekodi.
Nigeria ina rekodi nzuri kiasi ambapo mwaka 1994 iliwahi kuifunga Bulgaria mabao 3-0 nchini Marekani ukitilia maanani kuwa Bulgaria walizifunga Ugiriki, Argentina, Mexico na Ujerumani katika mashindano hayo.
Tangu aondoke kocha Clemens Westerhof aliyeijenga timu ya Nigeria mwaka 1994 timu hiyo imefundishwa na makocha maarufu kama Jo Bonfrere, Philippe Troussier, Bora Milutinovic na Berti Vogts.

Nigeria imeandika pia historia baada ya kushinda mashindano ya vijana ya FIFA chini ya miaka 17 ya mwaka 1985, 1993 na 2007 pamoja na ubingwa wa olympiki mwaka 1996.

GHANA

Ghana wapo katika kundi la D pamoja na Australia, Ujerumani na Serbia. Ghana ndio timu pekee ya Afrika iliyovuka hatua ya makundi katika fainali za mwaka 2006 nchini Ujerumani na pia imekuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kufuzu kwa fainali hizi za Afrika Kusini. Ghana wana matumaini makubwa ya kutaka kufanya vyema katika fainali hizi licha ya kwamba hizi zitakuwa ndio gfainali zao za pili kushiriki. Timu yao ya taifa maarufu kama BLACK STARS wanaamini kwamba wana aina ya wachezaji wanaowza kufanya chochote uwanjani na kupata ushindi. Ghana imeshinda mashindano ya kombe la mataifa barani Afrika mara nne na pia kombe la dunia kwa vijana chini ya miaka 17 mara mbili na kuwa timu ya kwanza ya Afrika kushinda kombe la dunia la vijana chini ya miaka 20 baada ya kuifunga Brazil kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 2009. Ghana inaonekana kuwa tishio kubwa katika fainali hizi kwanza kufanyika barani Afrika.

Walivyofuzu.
Ghana wamefuzu kwa fainali hizi baada ya kushinda michezo yao minne ya awali wakiwa na rekodio ya kutofungwa bao lolote katika michezo yao ya makundi hadi walipokubali kipigo cha bao moja kwa bila kutoka kwa Benin, lakini kipigo hicho kilikuja wakati tayari wameshafuzu.
Ghana walizitupa nje Mali na Sudan kwa kuzifunga mabao 2-0 ktika mechi za kwanza huku Matthew Amoah akifunga goli kila mchezo.

Wachezaji nyota.
Licha ya kwamba Ghana inakosa wachezaji wazuri katika nafasi ya ushambuliaji kama zilizvyo nchi nyingi za Afrika lakini wanao wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kucheza sehemu ya kati wakiongozwa na Michael Essien. Kiungo huyo wa Chelsea mara nyingi hushirikiana na Sulley Muntari na nahodha wao Stephen Appiah.
Asamoah Gyan, Junior Agogo ambaye huenda akakosa fainali hizo kutokana na maumivu na Matthew Amoah mara nyingi ndio wanaoongoza safu ya ushambuliaji huku katika ulinzi wakiwepo John Mensah na John Paintsil wakimlinda golikipa wao Richard Kingson.
Kocha: Milovan Rajevac kutoka Serbia.

Rekodi:
Ghana ilikuwa ndio timu yenye wachezaji wenye umri mdogo katika fainali za Ujerumani na Asamoah Gyan alifunga bao la mapema zaidi katika fainali za FIFA ambalo alilifunga katika sekunde 68 katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Jamhuri ya Zcech likiwa ni goli la kwanza kwa Ghana katika fainali hizo.
Ghana ilipoteza baada ya kufungwa mabao matatu kwa bila na Brazil katika raudni ya pili ya mashindano hayo ya mwaka 2006.

XS
SM
MD
LG