Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 27, 2024 Local time: 03:29

Kudorora kwa uchumi wa dunia kunazusha wasi wasi


Kiwanda cha mahindi Venezuela inayokumbwa na matatizo ya kiuchumi
Kiwanda cha mahindi Venezuela inayokumbwa na matatizo ya kiuchumi

Rais wa benki ya dunia Jim Yong Kim, anasema kuwa anawasiwasi juu ya kudhoofika kwa uchumi wa dunia na bei za chini za mafuta. Vile vile alizungmzia kuhusu kashfa ya utumiaji wa akaunti za nje na watu tajiri, mara nyingi wakijaribu kuepuka kulipa kodi. Bw Kim alielezea wasiwasi wake kabla ya kuanza kwa mkutano wa maafisa wa ngazi za juu wa shirika la fedha duniani IMF na benki ya dunia hapa mjini Washington .

Uthabiti wa uchumi wa dunia ni jambo linalozusha wasiwasi mkubwa kwa mkuu wa benki ya dunia Jim Yong Kim. Akitaja ukuaji dhaifu duniani kote, na kushuka kwa bei za mafuta, kadhalika mmiminiko wa wakimbizi huko Ulaya, Bw Kim anasema, huduma za benki ya dunia imezidi kuhitajika.

Bw Kima anasema, wanakadiria kuwa watatowa mikopo ya takriban dola billioni 25 mwaka huu kwa mataifa yenye pato la kadri. Hio ikiwa takriban dola billioni 10 zaidi kuliko walivyopanga.

Makadiriyo hayo mepya yanafikisha ukopeshaji wa benki ya dunia kufikia zaidi ya dola billini 150, hio ikiwa idadi kubwa zaidi katika mkondo ambao hauna mzozo, katika kipindi cha miaka 4, katika historia ya benki hio.

Gharama ya kuijenga tena Syria pekee yake huwenda ikizidi dola billioni 180. Anasema, nchi zinazozalisha mafuta huwenda zikakabiliwa na ugumu kutimiza ahadi zao za kimataifa, huku bei za mafuta zikishuka kwa baadhi ya nchi na kuwa baina ya dola 80 hadi 90 kwa pipa.

Masuala mengine amabyo huwenda yakajadiliwa kwenye mkutano huo wa IMF na benki ya dunia hapa mjini washigton ni pamoja na athari ya kujitoa kwa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya, na wimbi la wale wanaopinga wahamaiji kuongezeka katika nchi zilizoendelea.

XS
SM
MD
LG