Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 10:22

Benki ya Dunia yasitisha utoaji mikopo kwa Uganda


FILE - Banki ya dunia ilisitisha utoaji wa mikopo kwa Uganda tangu mwezi Agosti mwakea 2016, 2016.
FILE - Banki ya dunia ilisitisha utoaji wa mikopo kwa Uganda tangu mwezi Agosti mwakea 2016, 2016.

Benki kuu ya dunia siku ya Jumatano ilitangaza kusitishwa kwa utoaji wa mikopo kwa serikali ya Uganda kutokana na kile ilichokiita matumizi mabaya ya mikopo ambayo imetolewa tayari.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, na Benki hiyo, usitishwaji huo ulianza kutekelezwa tarehe 22 mwezi Agosti.

World Bank imesema kuwa inatathmini upya masharti ya mikopo hiyo, pamoja na ripori za kukiuka kanuni zilizotolewa.

Taarifa hiyoilieleza kuwa kumekuwa na visa vya kucheleweshwa kwa miradi iliyofadhiliwa na benki hiyo, udhaifu katika utekelezaji wa baadhi ya kanuni na kucheleweshwa ka malipo.

Hata hivyo benki hiyo imesisitiza azima yake ya kuendelea kufanya kazi na serikali ya Uganda , na wadau wengine, ili kuhakikisha kuwa miradi iliyoifadhili, itakuwa na matokeo mema ambayo yatawafaidi wananchi wa Uganda, hususan raia walio maskini na wanyonge.

XS
SM
MD
LG