Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 00:11

Wanawake kupinga kunyanyaswa Sudan Kusini


Wanawake Sudan Kusini wajifunza kutengeneza vinyago vya kuuza sokoni.
Wanawake Sudan Kusini wajifunza kutengeneza vinyago vya kuuza sokoni.

Watetezi wa haki za wanawake kutoka jimbo la Imatong wamesema watatumia siku 16 za uwanaharakati kuzungumza moja kwa moja na wanaume kuhusu kusambaa kwa manyanyaso ya kingono dhidi ya wanawake nchini Sudan Kusini.

Vile vile wanakusudia kutumia siku hizo 16 kuishinikiza Serikali kuteuwa wanawake zaidi kwenye nyadhifa za Serikali kuu na Serikali za mitaa ili waweze kuwa na ushawishi kwenye maamuzi na utungaji sera.

Wanaharakati hao wanasema kuwa vitendo vingi vya unyanyasaji wa kingono vinatekelazwa na wanaume na wale wanaotenda ubakaji wa genge na vitendo vingine vya ngono dhidi wanawake na wasichana mara nyingi huachiliwa huru kwa kuwa wanaume wenzao wanashikilia nyadhifa nyingi za kutoa maamuzi.

Wanawake hao wamesema kuwa utawala kandamizi ulioko Sudan kusini hautabadilika mpaka pale wanawake zaidi watakapoteuliwa kuwa machifu, kamishna wa kaunti na wakurugenzi kwenye wizara za Serikali.

XS
SM
MD
LG