Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 23:48

WMO yatabiri kurejea kwa mvua katika pembe ya Afrika


Wanawake na watoto huko kusini mwa Somalia wakipokea chakula kwenye kituo kimoja cha Mogadishu, hali hii imetokana na ukosefu wa mvua uliosababisha njaa katika pembe ya Afrika
Wanawake na watoto huko kusini mwa Somalia wakipokea chakula kwenye kituo kimoja cha Mogadishu, hali hii imetokana na ukosefu wa mvua uliosababisha njaa katika pembe ya Afrika

Idara ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa inatabiri kurudi kwa mvua za kawaida au zilizopita kiwango cha kawaida katika pembe ya Afrika

Idara ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa inatabiri kurudi kwa hali ya mvua za kawaida au mvua zilizopita kiwango cha kawaida huko kusini mwa Somalia katika eneo lililokumbwa na njaa.

Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani-WMO, lilisema utabiri wake uliotolewa Jumatano ni kwa kipindi cha mwezi wa Septemba hadi Disemba, ambapo ni msimu muhimu wa mvua kwa eneo la kusini ya Somalia na maeneo mengine ya ikweta katika pembe ya Afrika.

Pembe ya Afrika inataabika na ukame mbaya ambao umesababisha zaidi ya watu milioni 12 kuhitaji msaada wa chakula.

Shirika hilo la hali ya hewa linatabiri uwezekano wa kuongezeka mvua juu ya kiwango cha kawaida huko kaskazini-mashariki ya Tanzania, kusini ya Somalia, mashariki, kati kati na pwani ya Kenya.

Inatabiri mvua za kawaida au chini ya kiwango cha kawaida huko kaskazini ya Somalia, kaskazini-magharibi ya Kenya na mashariki na kusini ya Ethiopia.
Idara ya hali ya hewa inasema kwamba katika baadhi ya maeneo ya pembe ya Afrika, mwezi Septemba hadi Disemba sio msimu halisi wa mvua na kwamba katika maeneo hayo huwenda kutakuwa na upungufu wa ukame.

WMO inasema ubashiri wake ulifikiwa kwenye mkutano wa watabiri wa hali ya hewa wa Afrika mashariki na kimataifa mjini Entebe nchini Uganda wiki iliyopita.

Umoja wa Mataifa ulitangaza baa la njaa katika maeneo sita ya kusini mwa Somalia hapo Jumatatu. The Famine Early Warning Network inasema mvua finyu katika mwaka uliopita zilisababisha uzalishaji mbaya wa mazao ya mwaka kwa takribani miongo miwili.

Mamia ya wa-Somali wamekimbia nyumba zao wakitafuta chakula na maji, au kwenda kwenye makambi ya wakimbizi katika mji mkuu, Mogadishu, au kwenda kwenye kambi za wakimbizi nchini Kenya na Ethiopia.

Wataalamu wa hali ya hewa wanaonya kwamba licha ya juhudi za msaada za kimataifa, baa la njaa linaonekana kusambaa kuelekea sehemu nyingine za Somalia katika kipindi cha miezi michache ijayo.

XS
SM
MD
LG