Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 23:58

Wizara ya Sheria Marekani yatoa ripoti ya Polisi wa Ferguson, Missouri


Wizara ya sheria ya Marekani, imeeleza kwamba polisi wa Ferguson, Missouri, kwa kawaida hujiingiza katika vitendo vya ubaguzi wa rangi.

Hiyo ni kufuatia uchunguzi baada ya tukio la kupigwa risasi kijana mdogo mweusi Michael Brown, ambae hakuwa na silaha mwaka jana.

Ripoti ya wizara ya sheria inatarajiwa kutolewa Jumatano kwa mujibu wa shirika la habari la Associate Press.

Gazeti la The New York Times mwezi Januari liliandika kwamba wanasheria wa wizara hiyo walishauri serikali kuu kutofungua mashitaka ya haki ya kiraia.

Madai hayo yaliyofikishwa mahakamani dhidi ya afisa polisi mzungu aliyemuua kijana huyo mwezi Agasti baada ya majibizano yaliyosababisha ghasia na kifo.

Maafisa wanasema uchunguzi uliofanywa na idara ya upelelezi wa jinai FBI, katika tukio hilo ulionyesha afisa wa polisi Darren Willson, hakudhamiria kuvunja haki ya Michaela Brown, alipompiga risasi.

XS
SM
MD
LG