Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 12:51

Wizara ya Mambo ya Nje Iran yakanusha kuhusika katika tukio la kumshambulia Salman Rushdie

Mwandishi Salman Rushdie.(Picha na Evan Agostini/Invision/AP, Archivo)
Mwandishi Salman Rushdie.(Picha na Evan Agostini/Invision/AP, Archivo)

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran siku ya Jumatatu ilikanusha kuhusika kwa namna yeyote katika tukio la kumdunga kisu mwandishi Salman Rushdie.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran siku ya Jumatatu ilikanusha kuhusika kwa namna yeyote katika tukio la kumdunga kisu mwandishi Salman Rushdie.

Msemaji wa wizara aliwaambia waandishi wa habari kwamba Iran haioni kwamba hakuna mtu anayestahili kulaumiwa na kushutumiwa isipokuwa yeye na wafuasi wake.

Wakala wa Rushdie alisema Jumapili kwamba wakati mwandishi huyo anakabiliwa na hatua ya muda mrefu ya uponyaji hali yake inaelekea katika mwelekeo sahihi.

Mtoto wa Rushdie, Zafar Rushdie, alisema katika taarifa yake, ingawa majeraha yake ya kubadilisha maisha ni makubwa, ucheshi wake wa kawaida na ucheshi kwa jumla umebaki pale pale.

Mshambuliaji alimdunga kisu mara kadhaa Rushdie siku ya Jumapili alipokuwa karibu kutoa hotuba kuhusu uhuru wa kisanii katika Taasisi ya Chautauqua magharibi mwa jimbo la New York.

XS
SM
MD
LG