Wizara ya Fedha ya Afrika Kusini imesema itatekeleza hatua kadhaa za kupunguza gharama ili kudhibiti matumizi ya serikali, ikiwa ni pamoja na kusimamisha uajiri, baada ya upungufu katika ukusanyaji mapato.
Hazina, katika kukabiliana na hali mbaya ya uchumi imeelezea hatua hizo katika barua iliyotumwa kwa idara za kitaifa, mikoa na mashirika ya umma.
Gazeti la Sunday Times liliripoti mapema kwamba hatua hizo pia ni pamoja na kusitisha kutangaza kandarasi mpya za ununuzi kwa miradi yote ya miundo mbinu.
Ikijibu maswali ya Reuters, hazina ilisema mpango wa kupunguza gharama ulitokana na utendaji dhaifu wa uchumi na mapungufu katika ukusanyaji mapato.
Forum