Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 15:15

Shahidi wa kwanza kesi ya Bemba azungumza

Timu ya utetezi ya Bemba huko the Hague
Timu ya utetezi ya Bemba huko the Hague

Shahidi wa kwanza kutoa ushahidi kwenye kesi ya uhalifu wa vita dhidi ya makamu wa rais wa zamani wa Congo, Jean-Pierre Bemba, alisema Jumanne kuwa wanajeshi wa Bemba waliwabaka wasichana wadogo kijijini kwake huko Jamhuri ya Afrika ya kati mwaka 2002.

Shahidi ambaye wajihi wake ulifunikwa wakati anatoa ushahidi kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC, alisema katika tukio moja, mama mmoja alimpelekea mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka minane au tisa, ambaye alibakwa na wanachama wa Movement for the Liberation of Congo.

Alisema wanajeshi hao waliweka kambi karibu na makutano ya barabara katika kijiji chake, karibu na mji mkuu Bangui, na walianza kutenda ukatili. Alisema watu hao wanatambulika kwa sare zao.

Waendesha mashtaka wanasema Bemba anahusika kwa ubakaji, mauaji na wizi uliofanywa na wanajeshi wake aliowapeleka kumsaidia rais wa Jamhuri ya Afrika ya kati wa wakati huo Ange-Felix Patasse.

Timu ya utetezi ya Bemba inasema hakuwa na udhibiti juu ya wanajeshi wake mara walipokatisha mpaka kuingia Jamhuri ya Afrika ya kati na hahusiki kwa kile walichofanya.

XS
SM
MD
LG