Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 09:05

Wimbi la utekaji Uganda lawashitua wananchi


Uganda

Katika mwezi wa Februari gazeti la Monitor nchini Uganda tayari limefuatilia watu sita ambao familia zao zimeripoti kuwa wametekwa.

Katika mwaka 2017, sio chini ya kesi 24 za utekaji zimeripotiwa polisi. Kati ya hizi 24, mtu mmoja alikutikana amekufa, wengine 15 waliokolewa wakiwa hai na mpaka sasa 24 hawajulikani waliko.

Kwa mujibu wa gazeti hilo kikundi cha polisi kinachotumia ndege kufanya uchunguzi kimeripoti kuwa, washukiwa 27 walikamatwa, wengine 16 walifunguliwa mashtaka mahakamani na 11 wanaendelea kuchunguzwa.

Emilian Kayima, msemaji wa polisi, amesema kuwa vitendo vingi vya utekaji “ vinatokana na kuvunjika kwa mahusiano, yakipelekea jinai ya kuendelea kumshikilia mwenzake kimapenzi.”

Kayima ameongeza kuwa: “Kuna makubaliano ya kibiashara katika utekaji huu, na pia vitendo vya jinai. Tunawashauri watu wote kuripoti polisi iwapo yatafika masaa 24 na ndugu yako haonekani.

Ni muhimu kuwasiliana na maafisa wa polisi moja kwa moja ili kuepusha vitendo vya unyanyasaji visitokee kwa aliyetekwa au kuchelewesha kutoa taarifa bila ya sababu.

Jambo la tatu, unapotoa taarifa kwa haraka itapelekea pia kupata msaada kwa haraka. Ni jukumu letu sote kwa pamoja kupambana na vitendo hivi vya jinai na kuwachukulia hatua za kisheria watekaji hawa.”

Katika kile kinachoonyesha kuwa ni kuongezeka kwa vitendo hivyo vya utekaji kwa ajili ya kudai fedha nchini, familia nyingi zinaishi katika hali ya hofu ya kuwapoteza ndugu zao.

Kwa mfano baadhi ya familia kama vile ya Susan Magara, 28, na Philip Tumwebaze, 27, wameamua kufanya maombi kwa Mungu ili ndugu yao apatikane.

Na ni matumaini hayo hayo wamekuwa nayo wanafamilia wa Isaac Makubuya, 27, ambaye alitoweka tangu Februari 13 wakati alipopatamwito kwenda kutengeneza kompyuta mahali fulani Kampala, ambapo ameshikiliwa, rafiki wa familia hiyo ambaye hatuwezi kumtaja kwa sababu za kiusalama ametuambia.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG