Wimbi jipya la COVID-19 linaonekana kufukuta huko Ulaya wakati hali ya baridi ikianza, huku wataalam wa afya ya umma wakitahadharisha kwamba kulegalega utoaji wa chanjo na mkakanganyiko juu ya aina ya chanjo zinazopatikana huenda ikachangia kuzorotesha watu kupiga chanjo ya ziada yaani booster.
Virusi vya corona vya Omicron BA.4/5 ambavyo vilienea wakati majira ya joto bado vinahusishwa na maambukizi kwa kiwango kikubwa, lakini aina mpya ya virusi pia vinaenea. Mamia ya aina mpya ya Omicron inafuatiliwa na wanasayansi, maafisa wa Shirika la Afya Duniani (WHO) walisema wiki hii.
Takwimu zilizotolewa na WHO Jumatano jioni zilionyesha kuwa maambukizi huko Umoja wa Ulaya (EU) yamefikia milioni 1.5 wiki iliyopita, yakiwa juu kwa asilimia 8 ikilinganishwa na wiki moja kabla, licha ya kupungua kwa kushangaza kwa upimaji. Kimataifa, idadi ya maambukizi inaendelea kupungua.
Idadi ya wanaolazwa hospitali katika nchi nyingi zilizoko katika kanda ya mataifa 27, pamoja na Uingereza, imeongezeka katika wiki za karibuni.
Katika wiki inayoishia Oct 4, wagonjwa waliolazwa hospitali kutokana na COVID-19 wakiwa na dalili za ugonjwa waliongezeka kwa takriban asilimia 32 nchini Italia, wakati waliopokelewa wakiwa mahtuti waliongezeka na kufikia takriban asilimia 21, ukilinganisha na wiki moja kabla ya hapo, kulingana na takwimu zilizokusanywa na taasisi huru ya kisayansi ya Gimbe.
Katika wiki hiyo hiyo, waliolazwa hospitali kutokana na maambukizi ya COVID nchini Uingereza idadi ilionekana kufikia asilimia 45 ikilinganishwa na wiki kabla yake.
Chanjo zinazoendana na virusi vya Omicron zimezinduliwa Ulaya tangu Septemba, kukiwa na aina mbili za chanjo zinazokabiliana na virusi vya BA.1 na pia vya BA.4/5, lakini aina ya chanjo ya BA.1 ndiyo iliyoidhinishwa kutumika.
Maafisa wa Ulaya na Uingereza wameidhinisha aina mpya za chanjo za booster lakini kwa makundi maalum ya watu, ikiwemo wazee na wale wenye mifumo dhaifu ya kinga za mwili.
Linalofanya iwe vigumu zaidi ni “chaguo” la chanjo inayotumika kama booster, ambayo itaongeza mkanganyiko uliokuwepo, wataalam wa afya ya umma walisema.
Lakini utayari wa kupata chanjo nyingine, ambayo itakuwa ni ya nne au ya tano kwa baadhi ya watu, inazidi kuwa haina ushawishi.