Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 14, 2024 Local time: 10:44

Biden apona Covid, asifu ufanisi wa chanjo


Rais Joe Biden akizungumza katika bustani ya White House mjini Washington, Julai 27, 2022. Picha ya AP
Rais Joe Biden akizungumza katika bustani ya White House mjini Washington, Julai 27, 2022. Picha ya AP

Rais wa Marekani Joe Biden Jumatano amesema amepona ugonjwa wa Covid 19 akionekana hadharani kwa mara ya kwanza, ambapo amepongeza mafanikio ya utawala wake katika kupambana na janga la Covid.

Biden alionekana katika bustani ya White House akiwa amevalia suti na tai na miwani yake ya kujikinga dhidi ya jua, akionekana ametabasamu.

Biden aliruhusiwa kutoendelea kujitenga baada ya kupimwa mara mbili Jumanne na kukutwa hana virusi vya Covid.

“Nilipata nafuu haraka na ninajisikia vizuri,” Biden amesema.

“Muda wote nilikuwa nimejitenga, niliendelea kufanya kazi, kutekeleza majukumu yangu bila usumbufu wowote. Hii ni taarifa halisi ya wapi tumefikia katika vita dhidi ya Covid 19,” Biden ameongeza.

Biden alikutwa ameambukizwa virusi vya corona Alhamisi iliyopita. Alipata chanjo kamili na chanjo mbili za nyongeza maarufu booster.

Amewahimiza Wamarekani kuendelea kupata chanjo na dozi za nyongeza, maarufu booster, na kuendelea kuwa makini kutokana na ongezeko la aina mpya ya virusi vya Covid ambavyo vinaambukiza kwa haraka.

XS
SM
MD
LG