Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 22:25

WHO yabadilisha muongozo wa Zika


Shirika la afya duniani (WHO) linabadilisha ushauri wake kuhusu virusi vya Zika, likiwaeleza wasafiri kwamba yoyote ambaye ametembelea sehemu inayokabiliana na mlipuko huo kufanya ngono salama ama kuacha kufanya mapenzi kwa miezi sita.

Shirika hilo la afya la umoja wa mataifa lilitoa muongozo huo mpya hapo Jumanne, likirekebisha muongozo wa mwezi Juni ambao iliwashauri wanaume kufanya ngono salama ama kuacha kabisa kufanya mapenzi kwa wiki nane baada ya kutembelea nchi iliyoathiriwa na Zika.

Maboresho hayo yanakuja wakati uthibitisho zaidi ukizuka na kuonyesha namna mbu wanao ambukiza Zika wanaweza kuambukizwa kwa baina ya mtu na mtu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG