Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 07:23

WHO yaanzisha hatua zinazoenga kupunguza ghasia dhidi ya watoto


Watoto nchini Syria
Watoto nchini Syria

Shirika la afya duniani - WHO linaripoti kuwa takriban watoto billioni moja ikiwa ni nusu ya idadi ya watoto duniani, ni waathiriwa wa ghasia za kingono, kisaikologia na kimwili katika mwaka uliopita. WHO imeanzisha hatua ambazo inasema zinaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa ghasia dhidi ya watoto.

Watafiti wanakisia kuwa mtoto mmoja kati ya wanne wanaathiriwa na unyanyaswaji wa kimwili na takriban na msichana moja kati ya watano na mmoja kati ya 13 wanaume au wavulana ni waathiriwa wa unyanyasaji wa wa kingono.

Alender Butchart ni mratibu wa idara ya afya duniani anayeshughulika na kuzuia ghaisa. Anasema athari ya aina hizi za ghasia ni kubwa lakini hazitiliwi maanani.

Bw. Butchart anasema. kile tunachokiona ni mwanzo tu wa janga linalouwa. Kwa mfano, mauwaji ni miongoni mwa sababu tano kuu za vifo kwa watoto na katika baadhi ya maeneo au katika baadhi ya nchi ni namba moja au mbili. Ghasia dhidi ya watoto zinaweza kusababisha majeraha kama vile majeraha ya ubongo, na viungo vya ndani ya mwili, kuchomwa au vidonda na kadhalika, katika mamillioni ya kesi.Ghasia dhidi ya watoto mara nyingi hupelekea matatizo ya akili kama vile kuwa na huzuni na wasiwasi.

Butchart anasema ghasia dhidi ya watoto pia zinaweza kupelekea utumiaji mbaya wa pombe na madawa, kuvuta sigara na kufanya mapenzi kwa njia zisizo salama

Anasema tabia hatari kama hizo zinawaweka watoto hatarini baadae maishani kupata kiharusi, saratani, kisukati, magonjwa ya ini, HIV na ukimwi na magonjwa mengineyo.

Habari njema anasema Butchart , ni kwamba aina nyingi ya ghasia dhidi ya watoto zinaweza kuzuiliwa kupitia hatuwa zinazoshughulikia sababu zinazochagia hali hio. Anasema WHO na washirika wake 9 wamezindua mfumo wenye mikakati saba uwitao INSPIRE, ambapo kila herufi ya neon hilo inasimamaia mkakati mmoja. Anasema mikakati yote yamefanyiwa ukaguzi na yanaonekana kubuni matokeo mazuri.

Kwa mfanao anasema, herufi I inasimamia Implementation and Enforcement of Laws, yaani kuegezwa na kutekelezwa kwa sheria, kama vile kuzuia vijana kupata silaha . Anasema hii imeonyesha matokeo mazuri huko Afrika kusini, ambayo imefaulu kupunguza maelfu ya vifo vingi miongoni mwa vijana katika kipindi cha miaka 5.

Hatuwa nyengine ni pamoja na kubadili Imani na tabia kwa majukumu ya jinsia, na kubuni mazingira salama, msaada wa wazazi, kuboresha mapato, kutowa miradi ya matibabu kwa wakosaji vijana, na kuweka mazingira salama ya shule.

XS
SM
MD
LG