Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 06:35

WHO yasema Zika ipo kwa muda mrefu


Japokuwa maafisa wa afya ya jamii na watafiti wamefanikiwa katika kuelewa na kudhibiti virusi vya Zika, shirika la Afya duniani (WHO) linasema Zika itakuwepo kwa muda mrefu na lazima ishughulikiwe kama tatizo la muda mrefu.

Machache yalijulikana kuhusu Zika wakati WHO ilipotangaza ugonjwa huo kuwa ni tatizo la dharura la afya ya jamii ya kimataifa mwezi Febuari.

Toka wakati huo, idara hiyo ya Umoja wa Mataifa imejifunza kwamba, virusi hivyo vitaendelea kusambaa na kusababisha tatizo la “microcephaly” linalosababisha ubongo kutokuwa wa kawaida kwa watoto wachanga.

Lakini mkurugenzi mtendaji wa WHO wa mpango wa dharura za afya, Peter Salama, anasema suala kubwa kuhusu virusi hivyo bado halijulikani, na linahitaji kufanyiwa utafiti.

Kwa hiyo anasema mipango ya sasa ya dharura itabadilishwa na kuwa ya kati, na muda mrefu ya kazi ambayo itazungumzia masuala mengi ambayo hayajashughulikiwa.

Anthony Costello ni mkurugenzi wa Afya ya Uzazi, Watoto Wachanga, na Afya ya Watoto. Anasema Zika haitoweza tena kuwa dharura katika afya ya jamii katika namna inavyofahamika rasmi, lakini bado ni tatizo katika afya ya jamii na wasiwasi mkubwa duniani.

Shirika la afya duniani linahitaji dola milioni 112 kutekeleza mipango ya Zika mpaka mwakani.

Mpaka sasa, imeshapokea dola milioni 50.

WHO inasema inajipanga kufanyakazi kusaidia nchi zinazopambana na virusi vya Zika.

Inasema itasaidia kuandaa mifumo ya uangalizi ili iweze kufuatilia na kutambua virusi na kuvifuatilia.

Na itafanya kazi na nchi kuboresha na kuimarisha mipango yao ya majibu ya kitaifa ya kupambana na virusi.

XS
SM
MD
LG