Gaya Gamhewage, mkurugenzi wa ulinzi na mwitikio wa udhalilishaji wa kijinsia ndani ya WHO amesema katika miaka miwili iliyopita, tasisi hiyo imeongeza nguvu katika kuzuia na kuitikia jambo lolote kuanzia matendo ya udhalilishaji, manyanyaso, na dhuluma za kijinsia.
Ameongeza kusema kwamba licha ya hyo bado idadi ya shutuma hizo inakwenda juu kwa sababu nyepesi ambayo yeye anaamini ni kutokana na shutuma hizo bado hazijamalizwa.
Inakadiriwa kesi 83 za namna hiyo zimehusishwa na mlipoko wa 10 wa Ebola nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo asilimia 25 zinahusishwa wafanyakazi wa WHO.
Forum