Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 16:13

WHO  yaruhusu kampuni ya  Bavarian Nordic kutumia chanjo mpya ya mpox


Mhudumu wa afya akibeba trei katika kituo cha matibabu cha Mpox katika Hospitali Kuu ya Rufaa ya Nyiragongo, kaskazini mwa Goma Agosti 17, 2024.
Mhudumu wa afya akibeba trei katika kituo cha matibabu cha Mpox katika Hospitali Kuu ya Rufaa ya Nyiragongo, kaskazini mwa Goma Agosti 17, 2024.

Shirika la Afya Ulimwenguni-WHO  lilisema Ijumaa kuwa limeiruhusu kampuni ya  Bavarian Nordic (BAVA.CO), kutumia chanjo mpya ya mpox, chanjo ya kwanza  kuidhinishwa na shirika hilo ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo katika nchi zilizoathirika vibaya barani Afrika.

Uidhinishaji huo, unaojulikana kama sehemu ya kwanza unafungua njia kwa nchi zinazoendelea ambazo nyingi hazina teknolojia na rasilimali ya kufanya ukaguzi wa kina katika usalama na ufanisi wa chanjo kuweza kupata chanjo.

Mlipuko wa sasa ulianza mapema 2023 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo ina zaidi ya maambukizi 37,500 na vifo 1,451 kufikia Julai 28. Ugonjwa umeenea katika nchi 15 za Afrika Kwa mujibu wa CDC ya Afrika.

Forum

XS
SM
MD
LG