Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 09, 2024 Local time: 15:54

WHO yasema kiwango cha TB kimeshuka


Mfano wa vijidudu vya kifua kikuu-TB, ambavyo husambaa haraka kwa njia ya kukohoa
Mfano wa vijidudu vya kifua kikuu-TB, ambavyo husambaa haraka kwa njia ya kukohoa

Shirika la afya duniani linasema idadi ya watu wenye kifua kikuu na vifo kutokana na ugonjwa huo imepungua

Shirika la afya Duniani-WHO, linasema idadi ya watu wenye kifua kikuu imepungua na kwamba idadi ya vifo kutokana na kifua kikuu ipo chini katika kipindi cha miaka 10.

Ripoti mpya ya WHO inasema idadi ya watu milioni 8.8 walioambukizwa na ugonjwa wa mapafu mwaka jana imeshuka kutoka watu milioni tisa mwaka 2005.

WHO inaelezea kushuka huko kunatokana na ufuatiliaji wa karibu na ufadhili mkubwa wa kifedha katika nchi kubwa kama vile china na baadhi ya sehemu za barani Afrika na Latin Amerika.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, anasema kushuka huko ni mafanikio makubwa lakini anasema huu sio muda wa kuridhika. Anasihi uungaji mkono wa dhati uendelee kwa kusaidia kuzuia ugonjwa wa kifua kikuu katika kuzuia na kutoa huduma.

WHO iliripoti mwezi uliopita kile inachokiita tahadhari na kuongezeka haraka kwa dawa za kifua kikuu ambazo zinakaidi tiba huko ulaya.

Kifua kikuu kinasababishwa na vijidudu ambavyo vinaharibu mishipa miembamba ya mapafu. Ni hatari na unasambaa haraka kwa njia ya kukohoa.

XS
SM
MD
LG