Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 08:01

WHO kufikisha misaada Tigray


Shirika la afya duniani (WHO) Jumatatu, limezungumzia matumaini kwamba msaada wake wa kuokoa maisha utawasili katika mkoa wa Ethiopia wenye vita wa Tigray.

Msaada huo utafika katika siku zijazo, baada ya pande zinazo hasimiana kukubaliana kuratibu misaada ya kibinadamu.

Serekali ya Ethiopia, na waasi wa Tigray, walikubaliana Jumamosi, kufanikisha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu yote inayo hitajika.

Hii ikiwa ni sehemu ya makubaliano yaliyo afikiwa mwanzoni mwa mwezi ya kumaliza vita vibaya vya miaka miwili katika mkoa wa Kaskazini.

Ilipo ulizwa lini misaada inatarajiwa kuwasili, WHO imeliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya barua pepe kwamba inatarajia kupatikana kwa watu wote walio katika mahitaji katika eneo hilo katika siku zijazo.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema linatumai kutoka chakula kwa watu wa huko, dawa za kuokoa maisha, kurejesha vifaa vya matibabu katika vituo vya afya, kuwapatia watoto chanjo muhimu na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.

XS
SM
MD
LG