Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:13

Je, Antonio Guterres ni nani?


Antonio Guterres ana umri wa miaka 67 na aliwahi kuhudumu kama waziri mkuu wa Ureno kwa miaka kumi na kama mkuu wa UNHCR kwa miaka kumi.
Antonio Guterres ana umri wa miaka 67 na aliwahi kuhudumu kama waziri mkuu wa Ureno kwa miaka kumi na kama mkuu wa UNHCR kwa miaka kumi.

Antonia Guterres, ambaye siku ya Alhamisi alithibitishwa kama Katibu mkuu atakayechukua nafasi inayoshikiliwa kwa sasa na Ban Ki Moon, Galizaliwa mnamo mwaka wa 1949 na kusomea somo la phisikia katika chuo cha Superior nchini Ureno kabla ya kuwa profesa na kuanza kazi ya uadhiri mnamo mwaka wa 1971.

Lakini Guterres, ambaye amenukuliwa akisema kuwa ni wa imani ya Kikatoliki, hakufunza kwa vyuo vikuu kwa muda mrefu. Baada ya miaka milwili, alijitosa kwenye siasa, na kujiunga na chama cha Socialist Party, mwaka wa 1974.

Mnamo mwaka wa 1992, alichaguliwa kama katibu mkuu wa chama hicho cha Socialist Party, na miaka mitatu baadaye akachaguliwa kama Waziri mkuu wa Ureno. Alishikilia nafasi hiyo kwa miaka kumi…kutoka mwaka wa 1995 hadi mwaka wa 2005.

Guterres, ambaye anazungumza kwa ufasaha lugha nne, Kiingerea, Kireno, Kifaransa na Kispania, alijitosa kwenye uwanja wa diplomasia, na kuwa mkuu wa shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, wadhifa amaboi alishikilia kwa miaka kumi, hadi mwaka uliopita wa 2015.

Uongozi wake katika shirika hilo umetajwa kama ulioleta mabadiliko mengi hasa kwa sababu ni kwenye kipindi hicho ambapo wakimbizi kutoka nchi kama vile Syria, Yemen, Afghanistan, Somalia na Sudan Kusini waliongezeka.

Alipunguza wafanyakazi katika makao makuu ya shirika hili mjini Geneva, lakini akaimarisha uwajibikaji kwa kwa kuhakikisha kuwa maafisa wa shirika hilo, wananafika kwenye maeneo ya matukio na majanga haraka iwezekanavyo, na kutoa huduma za dharura kwa waathiriwa, huku pia akiimarisha usalama wa wafanyakazi hao.

Guterres ana watoto wawili kutoka kwa ndioa yake na mkewe wa kwanza, aliyefariki mnamo mwaka wa 1998. Alioa mke wa pili mnamo mwaka wa 2001.

Guterres ameonekana kupendwa na wengi katika baraza la usalama la umoja wa mataifa, kwa sababu kitendo hicho cha kuja pamoja kwa wawakilishi jhao, huwa ni nadra, wakatiu wa kupiga kura kwa maswala muhimu ya umoja huo, ulio na mataifa wanachama 193.

XS
SM
MD
LG