Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 19:23

WHO inafurahia usambazaji chanjo ya COVID kwenda Afrika unaleta matumaini


Wauguzi wa Afya wakionesha sanduku la chanjo ya COVID ya AstraZeneca huko Nairobi, Kenya, March 4, 2021.
Wauguzi wa Afya wakionesha sanduku la chanjo ya COVID ya AstraZeneca huko Nairobi, Kenya, March 4, 2021.

Mkurugenzi wa WHO kwa eneo la Afrika, Matshidiso Moeti anasema takribani dozi milioni 10 za chanjo zimewasilishwa kwa nchi 11 wiki hii na anatarajia kiasi cha nusu ya nchi zote barani humo zitapokea chanjo ya COVID-19 katika wiki kadhaa zijazo

Shirika la afya Duniani-WHO linasema usambazaji wa chanjo ya COVID-19 katika nchi za afrika unaongezeka na kutoa ishara zenye matumaini kwamba idadi kubwa ya watu watapata chanjo ifikapo mwishoni mwa mwaka. Takwimu za hivi karibuni zinaonesha idadi ya maambukizi barani Afrika zipo zaidi ya milioni 3.9 na vifo takribani laki moja.

Takwimu zinaonesha janga la COVID-19 kwa ujumla linapungua katika nchi nyingi za barani Afrika. Hata hivyo maafisa wa shirika la afya Duniani-WHO wana hofu kutokea tena kwa kesi siku zijazo wakati shinikizo linaongezeka la kulegeza masharti yaliopo. Wanataja kuongezeka kwa kesi za COVID-19 katika nchi 10 kama dalili ya wasi wasi.

Wakati huo huo, kuongezeka kasi ya usambazaji wa chanjo barani Afrika kunatoa matumaini. Mkurugenzi wa WHO kwa eneo la Afrika, Matshidiso Moeti anasema takribani dozi milioni 10 za chanjo zimewasilishwa kwa nchi 11 wiki hii na anatarajia kiasi cha nusu ya nchi zote barani humo zitapokea chanjo ya COVID-19 katika wiki kadhaa zijazo.

Mpango wa COVAX umerahisisha usambazaji chanjo barani Afrika
Mpango wa COVAX umerahisisha usambazaji chanjo barani Afrika

Anasema nchi nyingi zitakuwa na program za chanjo zinazoendelea ifikapo mwishoni mwa mwezi huu wa Machi. Moeti anasema mpango wa COVAX unalenga asilimia tatu ya idadi ya watu wakati unaanza utoaji chanjo huko Afrika. Lakini anaongeza kuwa lengo la COVAX ni kuongeza idadi hiyo na kuwafikia asilimia 20 ya idadi ya watu ifikapo mwishoni mwa mwaka.

“Anasema tumefurahi sana kwamba Umoja wa Afrika unafanya kazi kupitia wanunuzi wake, jopo kazi la wanunuzi wa chanjo linalenga kuhakikisha kuwa ifikapo mwisho wa mwaka, chanjo ya kutosha imenunuliwa na inapatikana kwa nchi kufikia asilimia 60 ya idadi ya watu”

Ifikapo mwisho wa mwaka, Moeti anasema anatarajia kufikia kiwango cha kufikisha chanjo katika nchi za kiafrika, kwamba sio tu kwa kupunguza magonjwa na vifo, lakini pia kuanza kupunguza kasi ya kusambaa kwa virusi vya Corona.

Kwa maneno mengine anasema anatumai bara hilo litafanikiwa kufikia kile kinachoitwa kinga ya kupunguza magonjwa ya kuambukiza katika jamii.

XS
SM
MD
LG