Maafisa wa misaada wanasema mahitaji ya kibinadamu yanahitajika sana, na wachambuzi wanasema hakuna suluhisho rahisi kutokana na wasiwasi unaoongezeka.
John Kirby, mkurugenzi wa mawasiliano ya ulinzi ya baraza la usalama wa taifa la Marekani amesema wamezungumza na maafisa wa Israel, kuhusu mahitaji yanayo endelea ya kibinadamu kwa ajili ya watu wa Palestina, ambao ni waathirika vilevile.
Maafisa wa White House, wamesema wiki hii kwamba wanazungumza na Misri, kuhusu uwezekano wa njia ya misaada.
Kuna vituo viwili tu rasmi vya kutokea Ukanda Gaza, ambapo Israel, Jumanne ilishambulia kituo kikubwa kinachokwenda mpaka Misri.
Forum