Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 07:10

White house yajibu ukosoaji kuhusu kuuwawa Bin Laden


Rais Barack Obama ajibu ukosoaji kuhusu mashambulizi ya yaliomuuwa Osama Bin Laden.

Obama asema utawala wake hauningizi siasa kwenye mashambulizi ya kumuuwa Bin Laden.

Rais wa Marekani Barack Obama anasema utawala wake hauingizi siasa kwenye mashambulizi yaliomuuwa Osama Bin Laden , na kupinga ukosoaji kwamba White house inajitumbukiza katika kusheherekea kupita kiasi juu ya kifo cha kiongozi huyo wa ugaidi.

Akizungumza siku kadhaa kabla ya maadhimisho ya mwaka wa kwanza tangu mashambulizi ya makomandoo yaliomuuwa kiongozi wa Alqaeda Osama Bin Laden, Bw.Obama alisema jumatatu kuwa kuna wengine ikiwa ni anaonyesha wazi kumlenga mpinzani wake katika uchaguzi wa Novemba ambao wamebadili misimamo yao juu ya kufanya jambo kama hilo.

Bila kumtaja Romney kwa jina Bw.Obama alipendekeza kuangalia maelezo ya siku za nyuma ya watu juu ya suala hilo. Romney alisema miaka kadhaa iliyopita kuwa haikuwa na maana yeyote kutumia fedha nyingi kumfuatilia mtu mmoja, lakini Jumatatu alisema kuwa angeagiza Bin Laden auwawe.

XS
SM
MD
LG