Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 12:52

White House inafanya juhudi kuwaondoa madaktari waliokwama Gaza


Timu ya madaktari 19 wakiwemo wamarekani 10 wamekwama Khan Younis huko Gaza
Timu ya madaktari 19 wakiwemo wamarekani 10 wamekwama Khan Younis huko Gaza

Timu ya wataalamu 19 wa afya wakiwemo Wamarekani 10 imekataliwa kuondoka Gaza baada ya kutoa huduma za matibabu

Utawala wa Biden unafanya kazi ya kuwaondoa madaktari wa Marekani kutoka Gaza baada ya Israel kufunga kivuko cha Rafah, White House imesema Jumatano.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema mapema wiki hii kwamba serikali inafahamu kwamba madaktari wa Marekani hawakuweza kuondoka Gaza, baada ya taarifa ya Intercept kuripoti kuwa zaidi ya madaktari 20 wa Marekani na wafanyakazi wa afya walikwama huko Gaza.

Taasisi ya Madaktari wa Marekani wenye asili ya Palestina, shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake nchini Marekani, ilimesema Jumatatu kuwa timu yake ya wataalamu 19 wa afya, wakiwemo Wamarekani 10, imekataliwa kuondoka Gaza baada ya kazi za wiki mbili za kutoa huduma za matibabu katika European Hospitali huko Khan Younis, mji ulio karibu na Rafah kusini mwa Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG