Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 14:34

WFP yaomba dola milioni 426 za kupambana na njaa Sudan Kusini


Watu wachukua chakula kilichoangushwa kwa ndege Sudan kusini
Watu wachukua chakula kilichoangushwa kwa ndege Sudan kusini

Shirika la chakula duniani WFP Jumanne limeomba msaada wa dola milioni 426 ili kutoa msaada wa chakula kwa mamilioni ya familia nchini Sudan kusini ambako vita na mafuriko zimewaacha kwenye hatari ya kuangamia. 

Akizungumza na wanahabari mapema Jumanne, mkuu wa miradi ya WFP nchini humo Adeyinka Badejo alisema kwamba tayari kuna tatizo kubwa nchini humo, hata hivyo anasema kuna haja ya kurejesha msaada wa chakula cha dharura ili kuzuia watu kuangamia kutokana na nja na ukame.

Ili kufikia malengo hayo amesema kwamba dola milioni 426 zinahitajika katika kipindi cha miezi 6 ijayo. Bajedo wakati akiwa mjini Juba amesema kwamba Sudan kusini inashuhudia mwaka wenye njaa zaidi tangu kujipatia uhuru wake. Amesema kwamba baadhi ya masuala yaliopelekea hali hiyo ni pamoja na mizozo ya kisiasa, mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababisha mafuriko kwa miaka mitatu mfululizo pamoja na kuporomoka kwa uchumi kufutia janga la corona, ikizingatiwa pia mzozo unaoendelea nchini Ukraine.

Kutokana na ukosefu wa msaada wa kutosha na kuongezeka mahitaji WFP ililazimika kusitisha kazi zake za kuwasaidia watu milioni 1.7 mwezi wa April. Badejo ameongeza kusema kwamba taifa hilo lisilo na bandari linaelekea mwaka wa nne wa mafuriko ambayo huenda yakalazimisha takriban watu laki 6 kuondoka makwao.

XS
SM
MD
LG